Lyrics: Roma – Nipeni Maua Yangu Ft Abiud

Download | Fast Download

Download Roma – Nipeni Maua Yangu lyrics, audio mp3

Roma Mkatoliki, is a rapper artist from Tanzania and has released a brand new song tagged “Nipeni Maua Yangu”.

Listen & Share

Lyrics

Tumekumisi Roma

Rudi Nyumbani

Uwatetee Wanyonge ndugu zako

Uwakumbushe

Sasa sijui nianzie wapi kifuani nimebeba mengi

Na sitotenda haki nisiposema hiki sipendi

Hiki napenda kile sitaki mambo ya kishenzi

Tanzania haijaezekwa bati na wamekula pesa ya ujenzi

Yaani nchi wanaifanya mti mjenzi anauona mbao

Ndege ataona makazi mkulima ataona mazao

Mganga atauona dawa na mpishi atauona kuni

Ataemiliki mwenye power sisi atatusagia kunguni

Na ukisema hawatufai wanakuumiza uwe mpole

Yaani wanaangua papai kwa kutumia gobole

Mnatumia nguvu kubwa kwenye mambo madogo

Jeshi gani mpaka leo mmeshindwa kumjua kigogo

Tukiongelea kutekwa eti tunarudia ajenda

Hamjibu mnakwepa mbona mama anarudia kilemba

Nchi gani raia akihoji mnasema anakosoa

Na akikosoa anatukana serikali hii sio poa

Haya basi tuseme mko sawa na mna nia nzuri na sisi

Mbona vyuma vimekaza halafu mama anaificha grease

Mara mkapandisha tozo kampeni mkono hatuwaungi

Si tulihoji mkajibu kwa dharau tuhamie Burundi

Tatizo mkishaapishwa tu mnawaza uchaguzi ujao

Hamuwazi njia mbadala ya kumlinda mkulima na mazao

Sasa Iringa si tuna maitu halafu tuspick twaagiza china

Manaake hapo kwanza ncheke yaani bongo kikubwa uzima

Sa mnatuambia tujiajiri mbona nyinyi hamkujiajiri

Okay nikupe bodacyangu kisha we unipe uwaziri

Nikukabidhi vyeti vyangu hangaika navyo mwezi mmoja

Niko pale nakujgoja uje tuongee lugha moja

Mi sio CCM sio Chadema hili niliweke wazi

Ila ukiweka CCM na Andazi ntachagua Andazi

Simuamini mtawala na mpinzani simsadiki

Maana wanaendelea kukatika huku deejay kauzima Mziki

Na inaniuma kuona msomi wa degree tatu

Nashindwa kumpa ajira sasa anauza nyanya karatu

Sasa sijui mtaniua nikimshikia mama shilingi

Maana hata inyeshe mvua mnasema anaupiga mwingi

Na ninamkubali na nitamng’ata sikio kama hujui

Wanaomkosoa ndo wanampenda wanaomsifia ndo maadui

Ili wapate teuzi ndo wanamlamba miguu

Wakimpamba hawamsaidii Amiri Jeshi Mkuu

Tunakupenda Roma Tunakumiss Roma

Rudi Nyumbani Roma Utusemee

Tunakupenda Baba Tunakumiss Mwana

Tunakukumbuka sana

Hivi hamjasikia tetesi kuwa remote iko msoga

Si huku mageng imedoda magogoni imenona

Watu tatu ndani ya track moja wamekalia kigoda

Ngolo Kante anampa Mbape cross anafunga Pogba

Hii nchi ina wenye nchi walanchi na wananchi

Na kuendelea kuwachagua ni kwenda na mchanga mbichi

Tuwajaribu wapinzani watawala si wameshapata

Ugoro umewaingia puani sasa ona wanapiga chafya

Wanatumia dollar kubaki kuongoza dola

Watawafunga watapora wataua watahonga vijora

Karatasi tunaibiwa za kura kwenye sanduku

Kwa hiyo mnatuonyesha ziwa huku mmeziziba chuchu

Okay kura ziko 300 na kuna watu mia kwa jimbo

Na kituoni hakukua na watu halafu wameshinda kwa kishindo

Sa kama Askofu mfufua watu ameiba kura za wapinzani

Je atashindwa kuiba sadaka za kura kanisani

Hii ni gani mchungaji akitaka gari twamchangia

Muumini akitaka gari anaombewa tunamsalia

Sa mchungaji tusimpe pesa tumuombeevna yeye pia

Tukae pale tusubiri miujiza ya wagalatia

Wabunge wengi mlishinda kwa hisani ya mwendazake

Mkipatacho muende Chato mkumbuke hata ndugu zake

Jimbo hili haliendelei cause mmemchagua mpinzani

Haya sasa mmeshinda kote fauluni huo mtihani

Turuhusu siasa za amani turudi zile enzi zetu

Uchaguzi sio siku moja ni mchakato wa muda mrefu

Mikutano ya nje na ndani ndo tunaimarisha chama

Daily mtulishe majani halafu sikukuu mtupe shawarma

Keki ya taifa ni kubwa tuache siasa za risasi

Mnawaonea wakishika dola watalipa kisasi

Tulipotoka ni mbali siasa za mwendazake

Msirudi msilale chali huku mnatutemea mate

Na BASATA msikie hili msije fungia huu wimbo

Kichwa kisicho na akili ni mzigo kwa shingo

Sawa tulinde maaduli ila tusiue wabunifu

Mtupende tunaokosoa kama mpendavyo wanaosifu

Wengine wamekuwa viongozi na mliwaona tu marapper

Hiphop ni mkombozi na sauti isiyo na mipaka

Ushauliza kwanini bega lipo karibu na kwapa

Usiondoke baki hapa usikie verse inayofuata

Tunakupenda Roma Tunakumiss Roma

Rudi Nyumbani Roma Utusemee

Tunakupenda Baba Tunakumiss Mwana

Tunakukumbuka sana

Nawashangaa vijana warembo na watanashati na nusu

Wanaosema bila mlengo eti siasa haiwahusu

Mwanasiasa anaweza amua tu na ukalala mahabusu

Mnakosea wadogo zangu na kamwe sitoruhusu

Siasa ndo inaamua sukari iuzwe shingapi

Na inapanga kaliua ni wapi wajenge zahanati

Na ijue tofauti ya mwanasiasa na mwanaharakati

Mmoja ndo mzalendo mwingine maslahi binafsi

Ntawafundisha kitu kabla hajawika jogoo alfajiri

Pesa unayonunua maduta mkate unaolipa bili

Hoja yake inamlipa Raisi Polisi Mbunge Waziri

So una haki ya kuwakosoa maana we ndo umewaaajiri

Tatizo hatuna ujasiri na akili tumekaza fuvu

Vipi nitafuzu kichwa suzuki engine ya Isuzu

Anayechelewesha msafara siku zote ni ng’ombe wa mbele

Ila anachapwa wa nyuma na ndo anayepiga kelele

Na mjenga katiba mpya sio BAWACHA wala BAVICHA

Eti wabonngo maji sio katiba mnawaficha

Haya sasa hayo maji yako wapi mbona hamuongei

Uko wapi umeme mmebugia kiazi cha mtoto

Mdomo unacheza sebene

Katiba iliyopo ni bora ipa ni bora kwa watawala

Ukipinga wanakupa keai na hauna hela kibatala

Kwa mwamvulu wa maendeleo wanahairisha mchakato

Mbona mkoloni alijenga miundombinu yote hapo

Na ili nchi iendelee inahitaji vitu vinne tu

Uongozi bora, siasa sadi, Ardhi na watu

Yanga na Simba ni wapinzani ila sio kwamba hawapatani

Maji yanayotoka mto msimbazi ndo yanayojaza jangwani

Na hiyo ndo amani tuitakayo sisi sio vurugu

Tunataka kuona Januari anamgongea fegi sugu

Hakika naacha glasi ya Bapa mezani anaenda msalani

Anamuachia mwigulu anarudi na anakunywa kwa amani

Na sio utani msipojifunza hapa ndo basi tena

Aliyesema aomgezewe muda bungeni ndo ameaga mapema

Wakamlisha asali kwa kisu akalamba akamwaga wino

Tangulia na dereva barua utaikuta chamwino

Mi nitakufa mimi ila ngoma zangu zitaishi

Na mtakuja na mashada siku yangu ya mazishi

Nipeni maua yangu niyanuse angali nipo hai

Nikiondoka mnikumbuke msilie bali mfurahi

Tunakupenda Roma Tunakumiss Roma

Rudi Nyumbani Roma Utusemee

Tunakupenda Baba Tunakumiss Mwana

Tunakukumbuka sana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *